Aliyekuwa Bi. Harusi
mtarajiwa, Elizabeth Terezia (32), mkazi wa Mbezi Beach, Kinondoni jijini Dar
es Salaam amebakwa, ameuawa kikatili na watu wasiojulikana wakati akitoka
katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe, Dar
linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, Kwa mujibu wa bwana harusi mtarajiwa,
Edefonce Sikwembe (42) ambaye ni mkazi wa Kunduchi, Dar tukio hilo la kinyama
lilijiri Oktoba 10, mwaka huu majira ya usiku wakati Elizabeth akirudi nyumbani
kutokea kanisani hapo. “Siku ya tukio
tulikuwa katika viwanja vya kanisa la Gwajima, nilimpigia simu mwenzangu
kumwambia nakwenda nyumbani kuandaa biashara ambayo ningeifanye kesho yake,”
alisema Sikwembe.
No comments:
Post a Comment