Yakiwa
yamebaki masaa machache wananchi wa Marekani waanze kupiga kura
kumchagua rais wa nchi hiyo kwa awamu nyingine, visa na mikasa ama
vituko vimezidi kutawala katika kampeni za uchaguzi huo labda ni mzuka
wa kuonesha hisia za watu tofauti tofauti kwa yule wanaemsapoti na
kumponda wasiyemsapoti.
Hivi
karibuni watu wanaosadikika kuwa ni wapinzani wa rais Obama wametoa
toilet paper zenye sura yake na T.P hizo zikasambaa maeneo ya
firestation huko Florida.
Ripoti
zinasema toilet paper hizo zimetolewa kujibu mashambulizi baada ya
mfanyakazi mmoja wa kituo hicho cha zimamoto aliziondoa sticker zote
zinazompinga Obama ambazo zilikuwa zimewekwa kwenye maeneo ya umma na
sio maeneo ya watu binafsi ama mali binafsi.
Hata
hivyo toilet paper hizo nazo zimeondelewa maeneo hayo na kupigwa
marufuku maeneo hayo ya Florida firestation kwa sababu ni maeneo ya umma
(public place) na sio maeneo binafsi.

No comments:
Post a Comment